woman holds crotch, needs toilet

Sababu 3 unahisi kukojoa wakati wa ngono

Je wanadada mumewahi kuhisi mkojo au kukojoa wakati wa lile tendo tamu?. Wewe unaona ni jambo la kawaida ? Likitokea hivyo utafanya nini?

Unaeza jisifia kwa makofi na kujipongeza kama limekutokea.sababu ya hili kufanyika ni mbili.kwanza ni kuwa ulisitisha tendo la ngono na kuenda msalani au pili,ulisusia na kuendelea na kufanya mapenzi.kuzingatia sababu zote mbili, kuhisi mkojo wakati wa ngono utokea kwa wanawake tu sababu ya uke wao.wanaume kwa kuwepo kwa uume wao wanaeza kukabiliana na changamaoto hiyo.

Sababu tatu unahisi kukojoa wakati unafanya mapenzi:

1. Presha kwa kifuko cha mkojo

Kwa maumbile, ya mbele na kifuko cha mkojo cha mwanamke ziko karibu sana ndio sababu yake ukifanya tendo la ngono shindikizo au presha kwa kifuko hicho humfanya mtu kusikia mkojo.ilhali kwa wengine hiyo haja huletwa na utekerenyo/hisia inayomuliki mtu wakati wakijamiana.

2. Aina au staili za kufanya mapenzi

Almarufu ‘dogi’ au msichana kuwa juu pia zinaeza kusimuwa mwnamke kuhisi kutaka kukojoa.kutokana na mgusano wa hizi staili/mbinu za kufanya mapenzi,zinaweza kufanya mtu kuhisi mkojo au hata kukojoa.

3. Kufikishwa kilele au mke kumwaga

Kukazwa na mkojo au kutaka kukojoa wakati wat endo la ngono inaeza kusababishwa na uwezekano wa mwanamke akitaka kumwaga ambapo mtu hujihisi kama anataka kukojoa.tusisahau pia wakati mwanamke amefika kilele akijamiana, hiyo hisia ya kutaka kukojoa inajitokeza.la kufahamu hapa ni ,kuwa kila mwanamke aweze kutofautisha hisia hizi mbili na ile ya kutaka kukojoa.

Je naeza kufanya nini nikihisi kukojoa?

La kwanza na la msingi,hakikisha umekojoa kabla ya tendo la ngono.mwanamke anapokojoa kabla ya kufanya mapenzi blade yake huwa tupu bila kitu na hii upunguza tukio la kuhisi mkojo wakati wa mechi/kufanya mapenzi na kumzuia mtu kufurahia.

Suluhu ya pili,wakati wa kufanya mapenzi jaribu kubadilisha mbinu/staili kwasababu kuna mbinu kadhaa uleta hiyo hali ya kuhisi mkojo.fauka ya yote haya, kwa ubora wa tendo hilo fanya iwe desturi wewe na mwenzako kuzifanyia majaribio aina kadhaa ndio mujuwe ni gani sahihi na isiyo na maudhi.

Jawabu la tatu, ni kuwa kuna wale wanaohisi kukojoa kabila ya kufika kilele au kumwaga wakati wa tendo.wale wako kundi hili, ni vyema kuthibiti hiyo hali na kutofautisha hisia ya kutaka kukojoa au ya kufikishwa kileleni na kumwaga.

Na tukizingatia sababu ya nne,fanya iwe ni desturi yako kuukaguwa mwili wako.juwa vile mwili wako ukujibu vipi wakati wa kufanya mapenzi? Unaeza tumia sex toys au mshiriki wako kuhafikia yote haya.

Kumalizia,kama bado hisia nib ado ni kero kwako, ni vyema kuwahusisha wahudumu wa afya.huwezi juwa pengine ni kuwepo kwa ugonjwa sanasana ukisika kuchomeka na  pengine kuwepo damu kwa mkojo au hata lengine lolote la kutaka ushughulikaji.

did you find this useful?

Tell us what you think

LoveMatters Africa

Blush-free facts and stories about love, sex, and relationships