cheerful lady look empty space white smile wear specs leopard print shirt

Kwa nini wanawake hupiga kelele wakati wa kudinywa?

Ni wakati gani wanawake hutoa kelele nyingi wakati wa kukulana? Wakati wamefika kilele? Au mtu wao anakaribia kushusha? Jiandae Kwa ukweli!

Kwa nini wanawake wengine hutowa yowe na kupiga kelele kitandani?

Mpenzi hodari, kufikia kilele, au kitu kingine chochote kile?

Majamaa, labda munafikiria kwamba anaomboleza na kupiga kelele kwa sababu wewe ni mpenzi hodari- unamsaga vyema, umemfikisha kilele kitamu ajabu. Samahani, fikiria tena. Hiyo siyo sababu kwa nini wanawake wana kelele kitandani, kulingana na matokeo ya utafiti kule Uingereza. Utafiti uligundua kuwa zaidi ya asilimia themanini na tano ya wanawake hufanya kelele nyingi ili tu wapenzi wao waongeze kujithamini.

Watafiti waliuliza zaidi ya wanawake sabini wanaoshiriki mapenzi ya jinsia tofauti ikiwa wana uwezekano mkubwa wa kufikia kilele wakati wa kunyonga, kupandishana nyege, au kufanya ngono. Pia walitaka kujua kiasi cha kelele walichotoa wanawake wale wakati wa shughuli hizo tofauti za ngono na sababu ilikuwa gani.

Wanawake wote wakati ule wa utafiti walisema walipiga kelele kitandani, iwe ni kupiga kelele kwa jina la mwenzi wao, kumwambia aende haraka au kwa bidii zaidi, au kuomboleza kwa raha. Lakini watafiti walipigwa na mshangao walipolinganisha jinsi wanawake walivyokuwa na kelele walipofika kilele.

Wanawake walikuwa na uwezekano mkubwa wa kufikia kilele wakati wa kupandishwa nyege – kama vile wapenzi wao walipowafanya ngono ya mdomo ikilinganishwa na ngono ya kuingiliana kimwili. Na sio kuwa wakati walipokuwa wamefika kilele ndipo walikuwa na uwezekano mkubwa wa kufanya kelele.

Kuhusiana: Jinsi ya Kusema Ikiwa Ameridhika Kitandani.

Kuinua nafsi yake

Linapokuja swala la kuomboleza na kupiga kelele, walipiga kelele nyingi zaidi walipokuwa wakifanya ngono, kabla na wakati wa kilele cha ngono wa wapenzi wao. Nam, sababu kuu ya wanawake wengi kufanya kelele kitandani ni kupandisha nyege wapenzi wao. Kwa kweli, karibu asilimia themanini walisema wanapiga kelele hata wakati wanajua hakuna nafasi ya wao wenyewe kufikia kilele.

Kupiga kelele hizo zote ni kuinua nafsi ya wenzi wao. Haimaanishi kwamba msichana naye anapata utamu wa juu zaidi. Kwa kweli, inaweza kumaanisha kinyume kabisa. Wanawake pia wanasema kwamba milio na mayowe ni njia mojawapo ya kuharakisha ngono wakati hawafurahii sana.

Kuhusiana: Je, wewe ni hodari kitandani?

Ndio, watafiti waligundua kuwa wanawake wanaweza na hutumia sauti zao kudhibiti jinsi mvulana wao anavyohisi wakati wa ngono na anapofikia kilele.

Na kwa nini wanafanya hivyo? ‘Kuendesha tabia zanaume kwa faida yao.

Watafiti wlisema kuwa ,Kuikuza nafsi ya mwenziwe kwa kupiga kelele nyingi kunaweza kusaidia kuimarisha uhusiano kati ya mwanamke na mpenzi wake. Lakini pia kuna faida ya kuharakisha kufika kilele kwa mvulana ikiwa mwanamke ana maumivu, kuchoka tu, au akiwa tayari kujipindua na kwenda kulala.

Ishara za kujificha.

Kwa hivyo nyie wanaume , ikiwa kweli mnataka kumfurahisha, msiende kwa mchezo mrefu, tafuta ishara za kujificha za furaha. Na kwa wasichana, ni vizuri kwenu kumshangilia hivyo, lakini msisahau kumwonyesha na kusema ni nini hasa kinakufanya uchizi kabisa…

Je, una kelele wakati wa kukulana? Je, unafanya makusudi, au hutokea tu? Acha maoni hapa chini au kwenye kurasa zetu za Facebook Love Matters Kenya.

did you find this useful?

Tell us what you think

LoveMatters Africa

Blush-free facts and stories about love, sex, and relationships