A ripe banana resting on half an orange

Ngono kupigika freshi inahitaji?

Kufanya ngono ile imeweza ni ile ambayo haiumuzi masela na ukiwa unapiga gemu, basi piga kitu ukutumia mbinu poa na uwe macho iskuletee kero la kuchomeka au kuchoma mtu na gonjwa la zinaa au pia kukanyaga waya.

Kila mchezaji katika hii fani ako na usemi wake kuna wale wa wa kushikashika mikono hapa na pale kwenye masehemu, kupigana denda wakipandishana kwiru na kuna yule mchezaji hodari wa mpaka jongoo aingie kwa mtungi

Sasa nawachanue ukisema kufanya mapenzi au imekulwa basi ni haya:

  • Kufanya ngono ya mdomo
  • Ya uke/nunu
  • Kuna ile ya jongoo aingia kwa  tupu ya nyuma.
  • Kutumia madoli  na vikaragosi vya ngono.
  • Wale wa kujipa raha kwa vidole au kutumia mkono.
  • Wale wa kusugua sehemu zao za siri kujipa raha.
  • Wale wa maneno ya kupandisha nyege
  • Wale wakubusiana/kunyonyana
  • Wale wa kupapasana na kutekerenyana kupandisha nyege
  • Wale wa BDSM kutumia mbinu aina aina kufungana, kutawalana, kunyenyekea na mengine

Hii list si kamili, je unajua mbinu gani nyengine?

Asikuambie mtu kitu, we juwa chochote unachofanya cha mapenzi kuna na hatari yake. Mbinu zote si salama kuna kupata gonjwa la zinaa ikachangia kupata hata na virusi vinavyo sababisha ukimwi na hata kupata boli. Njia nyengine kama Kupapasana ni salama mno,.

Kuna aina mbali mbali za kufanya mapenzi ambazo ni zasalama japo zinahusisha, mwili kugusana na sehemu nyeti zikawa na nyute au damu. Mlinda lango au mshambulizi anaweza kusambaza ngoma au gonjwa la zinaa.

Sasa kwa mshambulizi na mlinda lango kuna vile unaweza kupunguza hatari.mifano hai ni:

1. Tumia mpira/vaa sokisi kwa gemu

Hiyo gemu haitachafuka kamwe, kondomu inaokolea pakubwa, sema kuzuia mimba, magonjwa ya zinaa na hata huwezi sambaza virusi ukitumia kwa njia poa.isitoshe kondomu ziko tele hata bure wazipata.Hapa ni kwa wote hata wakuliwa nyuma.

2. Tumia bawa la meno/Plastiki

Kupigana Mate au denda kukipanda sana kuna majimaji hutoka na huwezi jua, umdhanie siye siku zote.Unapojihami na mabawa ya meno basi uko vizuri na salama kwani hivi kaka/dada vina weza hiyo kazi pasipo shaka upige denda bila wasiwasi na ujikinge na maradhi.

3. Vifaa na madoli ya shughuli vioshwe

Ukishafanya mambo yako na toys zako wale wana mitindo ya kileo,ni bora ziwe safi  maanake kama munazitumia wengi ,kusambaza virusi vya ukimwi au magonjwa ya zinaa itakuwa rahisi sana.Osha kwa kuzingatia miundo na aina za ngono . Japo ni njia salama ya ngono,usafi ni lazima na tuwache kutumia wengi chombo kimoja.

4. Kuwa na mshambulizi mmoja na mlinda lango mmoja

La muhimu sana ni kuepuka gemu maanake ndio salama na itakutoa kwa shaka la magonjwa ya zinaa na hata kupata virusi, mimba za mapema na mengineo.vile inatakikana kama huwezi ni kuwa na mshambulizi mmoja na mlinda lango. Hili pamoja na kupiwa kila mara na mawasilianona mwenzako kutapunguza uwezekano wa kupata ugojwa wa zinaa.

5. kufanyiwa uchunguzi kila wakati

Ili kuboresha kushiriki kimapenzi, la msingi sana ni kujuwa hali yako ya afya. Kutathmini uwepo wa magonjwa ya zina na kupata tiba iwapo una ugonjwa wa zinaa.Vilevile ni bora ukijiepusha na ngono iwapo una ugonjwa wa zinaa hado pale yule ameambukizwa ugonjwa wa zinaa amepona.

6. Kuwa macho, ulevi na ngono sio pozi poa

Utumiaji wa madawa ya kulevya au mastimu, ukishapiga zako uamuzi wako huwa si wewe ni ulevi wakuamulia. Vyema ni kutoshiriki mashambulizi kama akili si yako. Changamoto zake ni kibao sana, hutaweza kujiamulia kinga inayaostahili na kupata magonjwa ya zinaa au virusi vya HIV itakuwa rahisi.

Kiukweli, inapaswa mshambulizi na mlinda goli wasikizane kabla washiriki kwa mechi na si mambo ya  cha lazima au kutishiana maisha.

Oyee, utatuambiaje wewe juu ya mahusiano salama ambayo wewe unashiriki.kama unalo, basi tuzungumze kwa sehemu ya mapendekezo.

did you find this useful?

Tell us what you think

LoveMatters Africa

Blush-free facts and stories about love, sex, and relationships