woman holds crotch, needs toilet

Sababu 3 kuu unahisi kukojoa wakati wa kukulana

Wanawake, mmejisikia kukojoa wakati wa ile tendo tamu? Je, hii ni kawaida? Je  Unapaswa kufanya nini?

Piga makofi mara mbili ikiwa umewahi kuhisi hamu ya kukojoa wakati wa kukulana. Huenda ukasitisha ngwati ili kukimbilia bafuni au ukapuuza na kuendelea. Vyovyote vile, kuhisi kama unataka kukojoa wakati wa kujamiiana ni kawaida kabisa kwa watu walio na uke. Wamiliki wa mjulus wana utaratibu wa asili wa kukabiliana na suala hili.

Sababu tatu za kujisikia kukojoa wakati wa kukulwa:

1. Presha kwenye kibofu cha mkojo

Uke wako na kibofu cha mkojo uko karibu kabisa na hivyo ngono inaweza kuweka shinikizo kwenye kibofu chako na kukufanya uhisi unataka kukojoa. Katika baadhi ya matukio, hamu ya kukojoa huletwa na msukumo wa ndani kutoka kwa kupenya kwa mjulus.

2. Njia fulani za kukulana

Baadhi ya njia za ngono kama  ya mbwa au msichana juu inaweza kufanya baadhi ya wanawake wawe na hamu ya kukojoa. Aina ya msuguano kutoka kwa njia hizi wakati mwingine inaweza kuchanganya hisia zinazoendelea huko chini, na kukufanya uhisi kama unakwenda kukojoa.

3. Kufika kilele na kumwaga kwa mwanamke

Hamu ya kukojoa inaweza kuwa tu kwa sababu unakaribia kupata mwaga kwa mke ambao unaweza kuhisi kama kukojoa. Pia, wakati wanawake wanakaribia kufika kileleni, wanaweza kupata hisia hii pia. Ni muhimu kwa wanawake kutofautisha hisia za kuwa na mshindo na hamu ya kukojoa.

Nifanye nini ikiwa ninahisi kukojoa?

Kwanza, mojawapo ya suluhu rahisi ni kuhakikisha kwamba unakojoa kabla ya kukulana. Hii itahakikisha kwamba kibofu chako hakina kitu na pia kupunguza hofu ya kukojoa wakati wa kukulana ili uweze kufurahia gemu kikamilifu.

Pili, jaribu kubadilisha mkao wa ngono kwani baadhi ya misimamo huleta hamu ya kukojoa. Usiogope kujaribu na mwenzako ili kuona ni nafasi gani inakufaa zaidi.

Tatu, baadhi ya wanawake huhisi hamu ya kukojoa kabla ya kufika kileleni au kumwaga mwanamke. Ikiwa hii ndio sababu, unaweza kutaka kungojea na kuiweka hapo. Pia, kuwa na nia ya kutafuta tofauti kati ya hisia ya kuwa karibu na kuma na kutaka kukojoa.

Nne, Jipende na uchunguze mwili wako peke yako. Elewa jinsi mwili wako unavyohisi na kuitikia wakati wa vitendo vya ngono. Unaweza kutumia toi ama vifaa vya kujipa utamu wa ngono au unaweza kuchunguza na mpenzi wako.

Hatimaye, ikiwa unahisi kukojoa kila wakati wakati wa ngono, inashauriwa kuonana na daktari kwa sababu inaweza kuwa una hali ya kiafya. Hii ni hasa ikiwa pia unahisi kuchomeka, unaona damu kwenye mkojo wako, au dalili zozote za kukutia wasiwasi.

Je, umewahi kujisikia kama unataka kukojoa wakati wa kukulana? Je, unakabiliana nayo vipi?

did you find this useful?

Tell us what you think

LoveMatters Africa

Blush-free facts and stories about love, sex, and relationships