scared african man with orange shirt

Kufikishwa kilele bila mshusho (dry orgasm) 

Je ukijuwa kuwa kuna baadhi ya wanaume ambao ufikisha kilele wakati wa ngono bila ya kushusha mshusho (dry orgasm).

Upeo wa kujamiana baridi hutokea haswaa pindi mwanaume anafika kwa upeo war aha ya kujamiana  lakini yeye hatoi au kumwaga mshusho wowote.

Upeo wa kujamiana baridi inaeza kuwa ni tukio la ghafla/ kwa mda au likawa la kudumu na vile linatazamiwa kama lenye kutaka kutathminiwa,tukio hili linaweza kusababisha madhara ya uzalishaji kwa mume.kwa ukweli, pia wanaume wengi jambo hili huwaangusha mabega na motisha.

Ni nini husababisha upeo wa kujamiana baridi? (dry orgasm)

Sababu kuu ya tukio hili ni uwezekano wa mtu amepitia oparesheni  ya tezi dume (prostate gland surgery)  hii inahusisha kutolewa kwa  tezi (lymph nodes), au  pengine baada ya oparesheni yabkutolewa kwa blada kwa jina la utaaluma ni uondoaji wa uvimbe (CYSTECTOMY). Lakujuwa ni kuwa mawili haya yakifanyiwa mwanaume basi uwezo wake wa kumwaya/kushusha mshusho ni sufuri.

Kwa wengine upeo wa kujamiana baridi (dry orgasm) umfanyikia mtu pindu mwanaume amefanyia oparesheni ya kansa ya korodani (TESTICULAR CANCER) hii ni kwasabu ina athiri mishipa ambao uchangia uwezo wa mtu kufika kilele wakati wa ngono.

Wakati mwingine, utofauti wa maumbile ya mtu pia inaweza kuwa sabau kuu ya kilele baridi.

Kuwepo kwa marudio ya kufikishwa kilele, kwa mda mfupi pia inaweza kuwa ndio sababisho la kilele baridi.Wakati mwanaume anafikishwa kilele  kwa ufululizo wakati wa ngono,kiwango cha mishusho kinaweza kupunguwa ambapo pia mwili wa mtu utahitaji mda mwafaka kudhibiti ipate kiwango mwafaka  ya akiba  ya mishusho.Ikifika ni hivi, basi mtu asiwe na wasiwasi kwa sababu hali hii si ya kudumu maanake itachukuwa masaa na kila kila kitu kurudi pahali pake iwapo muhusika atapumzika.

Kwa kujumuisha, kuja uwezekano ukiwa katika matibabu wa kadha, kama vile shindikizo la damu ( high blood pressure) uvimbe au kupanuka kwa  tezi dume (PROSTATE ) na hali za magonjwa kama kama vile kisukari,kuzibika kwa njia ya mkojo, upungufu wa homoni amabayo husaidia mvulana kubalehe,maumivu katika uti wa mgongo tukimalizia na milipuko ya  ugonjwa wa kukacha kwa seli/tishu (SCLEROSIS) amabazo ni changizi kubwa kwa mtu kupata kilele baridi.

Jambo muhimu la kuzingatia inawezekana mishusho kwa bahati mbaya ikaingia kwa blade badala ya kupitia kwenye uume. Hali hii kwa kimombo hujulikana kama RETROGRADE EJACULATION na pia ikona utafauti na kielele baridi (dry organism) na utofauti si linguine bali hapa mshusho utoka ukipitia blade na si kwenye uume.

Tiba ya upeo wa kujamiana  baridi ( dry orgasm)

Japo tendo hili si la kumpa mtu wahaka, kuna umuhimu wa kujuwa ni kipi kimemsababishia mtu kuwa  hivyo na la msingi kufwatilia vile atapata matibabu kama kuna mtu anahisi utata.unapofika kwenye kituo cha afya muhudumu ataweza kukuchunguza na kukupa tiba au dawa ya suluhu kulingana na uzito wa hali yako.

Hatuwezi kukana kuwa kuna matukio  amabapo dry orgasm inatibika, na pia zisizotibika.Mwanaume mwenye hali hiyo imedumu basi bila shaka itaweza kumletea athari katika  afya yake ya uzazi na la kusikitisha kukosa kupata watoto.kuna pia nafasi ya dakitari kukupa njia mbadala yaw ewe kupata watoto na mchumbako.

Tusisahau kuzingatia kuwa mwanaume mwenye dry orgasm ako na uwezekano wa kushusha SPERM/MISHUSHO/MANII tofauti yake ni kuwa itachangia uwezekano wa kupata mimba zisizo na mipango au kuambukizana magonjwa ya zinaa.kwa kumalizia unashauriwa kutumia kinga wakati wowote kuzuia maambukizi  au mengine kutokea.

did you find this useful?

Tell us what you think

LoveMatters Africa

Blush-free facts and stories about love, sex, and relationships