Sisi wakufanya ngono ya mdomo je ubikira tunao?
Nilijikanya sana kuwa mimi, sipeani vitu mapaka ile siku nitasikia nimeiva na niko tayari kwa gemu, Mimi nitabaki na ubikira wangu.
Juzi juzi kuna huyu jamaa alifika mpaka chini chini kwenye vitu, nawaza sana. Je bado ubikira ninao?
Kwa mawazo ya kitamaduni, kuwa bikra inaamanisha mtu hajaingiliana kimwili na mwenzake. Kuingiliana kimwili kunaweza kuwa kupitia tupu ya mbele au tupu ya nyuma. Iwapo umechangayikiwa, hata kuingiza tu kichwa cha uume pia ni kuingiliana kimwili.
Ijapokuwa sisi husema ubikra unamaanisha, wewe hujawahi kufanya ngono yam domo ama yakupitia tupu ya nyuma, kuna maelezo kibao yakuchambua ngono. Hili linamanisha kuwa kueleza kwa uwazi ubikra si rahisi hivyo. Kwa jamaa wengine, ngono ya mdomo kwao inamaanisha washaupoteza ubikra. Kwa jamaa kama hawa kufanya tendo lolote la ngono ni kupoteza ubikra. Na kuna wale ambao kupeana nyuma na kutofanya ngono ya tupu ya mbele kwao wanadai bado ni mabikira.
Usiwaze, vile waelewa ubikira ni mawazo yako mwenyewe. Lakuzingatia ni kuwa, kuwa bikra ni kwa wote makaka na si mabinti pekee. Tupo?
Wale wa kitamaduni , ubikira wapotea tu pindi ukiingiwa mbele, na kufanya ngono ya mdomo hakupotezi ubikra. Hata kuna jamaa wengine amabo wanatumia ngono ya mdomo kuhifadhi ubikra wao.
Hata kama, je waweza fikishwa peponi na kumwaga?
Ndiyo, inawezekana kufika kilele cha ngono ama kumwaga kutokana na ngono ya mdomo hasa kiragwe cha binti ama uume unaposisimuliwa hata kam wewe ni bikra.
Lakukumbaka,hata kama ukila na mdomo sehemu nyeti hakutoi ubikira au kumpa mtu mimba, unaweza pata gonjwa la zinaa. Magonjwa ya zinaa yatakupata kama vile klamidia,malengelenge na kisonono . Hivyo basi ni muhimu kuweka kwa mpango kondomu zenye mafleva kwakina kaka na mabawa ya meno kwa kina dada.
Je bado wewe umekita hapo pakusema,mtu hatabaki bikra akifanya mambomambo na mdomo?. Kama una la kuambia watu. Sema nasi kwa sehemu ya mapendekezo.