young, puzzled business man thinking, deciding deeply something, finger on lips looking confused, unsure isolated grey wall background with texture. Emotion facial expression feeling

Je wanaume wanapaswa kukojoa baada ya ngono?

Inafamika wazi na wengi kuwa wanawake wanashauriwa kukojoa baada ya tendo la ngono ili waoshe kibofu cha mkojo na kutoa vidudu vyovyote vinayoweza  kuleta madhara. Na je, ikifika kwa wanaume kunaendaje?

Je wao pia yafaa wakojoe baada ya tendo la ngono? Na hayo yote yana faida yeyote  kwao? Hebu tulizungumzie hili jambo.

Ukweli halisi ni kwamba, wanaume hawahitaji kukojoa baada ya tendo la ngono. Sababu kuu ni kuwa wanaume wana urethra/mrija wa mkojo mrefu , hii inaleta ugumu wa bakiteria kuleta maambukizi kama kwa wanawake.

Wakati wa kujamiana/ngono bakiteria zinaweza kupenya kutoka kwa sehemu nyeti(genitals) zikipitia urethra/mrija wa mkojo mpaka kwa blade na kusababisha UTI/ maambukizi ya mfumo wa mkojo. Isitoshe, kimaumbile uwezekano wa kupata maradhi ya UTI/ maambukizi ya mfumo wa mkojo ni finyu mno kwani wao hupitisha mkojo kupitia urethra hivyo basi kuosha bakteria yeyote alioko mle ndani.

Unaeza soma kwa ziada- kwanini mtu huhisi kukojoa baada ya kufanya mapenzi?

did you find this useful?

Tell us what you think

LoveMatters Africa

Blush-free facts and stories about love, sex, and relationships