Yellow ripe banana wrapped in tape measure

Maumbo na ukubwa wa mboro au mjulusi

Uume huja kwa maumbo na saizi zote. Na zote zinaonekana tofauti: moja kwa moja, iliyopinda, ndefu, nene, nyembamba, waliotahiriwa, na wasiotahiriwa. Mmoja sio bora kuliko mwingine.

Ukiwa haujasimika, uume huwa na urefu wa kati ya sentimita 6 na 13. Iliyosimama kwa kawaida iko mahali Fulani urefu wa kati ya 7 na 17. Uume uliosimama wastani ni kama sentimita 12. Mjulusi mdogo hukua zaidi kwa saizi pindi inaposimika ukilinganisha na mjulusi mkubwa.

Baadhi ya wavulana na wanaume hutaniana sana kuhusu ukubwa wa mboro yao au uume wa watu wengine. Mara nyingi ni kwa sababu wanahisi kutokuwa salama, au kwa sababu wanataka kuonekana shupavu, au wanataka kufidia ukosefu wa maarifa.

Ikiwa unataka kupima uume wako, fanya ukiwa umesimika, upande wa juu upande ulio karibu na tumbo lako?

Ndizi katika ukubwa tofauti na maumbo zilizopangwa  wima

Je, ukubwa unajalisha?

Ikiwa una njulus mkubwa, haikufanyi kuwa mpenzi bora, na haimaanishi kuwa utakulana bora zaidi.

Wasichana au wanawake wanathaminii, mapenzi na kuridhika kwa uhusiano kuwa muhimu kama uume wa wenzi wao

ukubwa.

Kuhusiana: Je, Wanawake Wanapendelea mboro Kubwa?

Je, kondomu huja kwa ukubwa tofauti?

Ndiyo. Unaponunua kondomu, ni muhimu kupata zinazokufaa. Kondomu nyingi zimetengenezwa ili zitoshee wastani wa saizi za uume uliosimama (inchi 4.7 hadi 5.9 sentimita 12 hadi 17).

Kondomu

Kondomu tofauti katika maumbo na ukubwa tofauti

Kuhusiana: Maumbo na Ukubwa wa Uke: Je, Vyote Ni Sawa?

Je, watu kutoka makabila fulani wana uume mkubwa kuliko wengine?

Hakuna ushahidi kamili wa kuthibitisha kwamba makabila fulani yana mboo kubwa kuliko nyingine.

Walakini, mashirika mengine kama vile Mashirika ya Afya Ulimwenguni yameripoti kuwa kuna  tofauti kidogo ya kikabila kuhusu ukubwa wa uume uliosimama ama:

  • Asili ya Kiafrika ina uume mrefu na mpana kidogo
  • Wazungu wa asili ya Ulaya wana uume wa ukubwa wa kati
  • Asilia ya Waasia wana uume mwembamba kidogo na mfupi

Je, unaweza kujua urefu wa mjulusi wa mtu kwa ukubwa wa mikono au miguu yake?

Hapana. Hakuna uhusiano kati ya kuwa na saizi kubwa ya kiatu au mikono mikubwa na kuwa na uume mkubwa

Je, unaweza kufanya uume kuwa mkubwa kwa urefu au upana?

Hakuna mbinu zisizo za upasuaji ambazo zinaweza kufanya uume kuwa mkubwa zaidi.

Bidhaa ya njia nyingine za kukuza uume kama vile vidonge, kubeba uzani, na vifaa vya kunyoosha kawaida hazifanyi kazi muda mrefu.Na huenda zikaleta  hatari sana kwa afya yako.

Kuhusiana: Je, Kukuza Uume Hufanya Kazi?

Mboro ndogo ni nini?

Uume mdogo ni uume ambao hupima urefu wa chini ya inchi 2.75 sentimita 7 ukiwa umesimama. Hili hutokea ikiwa kiwango cha homoni ya kiume iko cha chini sana wakati mtoto anakua kwa tumbo la uzazi. Wavulana wengi na wanaume ambao wana wasiwasi wana mboro ndogo na ambao wanaona daktari hawana kweli kuwa na hali hiyo.

Mara nyingi, mjulus huonekana mdogo kuliko ulivyo kwa sababu umefichwa na mafuta karibu na sehemu za siri. Katika hali nyingine, ikiwa mvulana hajabalehe bado, uume wake unaweza kuonekana mdogo ikilinganishwa na ukubwa wake wa mwili. Hili si jambo la kuwa kukutia  wasiwasi , kwa sababu mara tu kubalehe kunapoanza, uume pia utakua kwa urefu na upana.

did you find this useful?

Tell us what you think

LoveMatters Africa

Blush-free facts and stories about love, sex, and relationships