Nini husababisha uchache wa mbegu za kiume?
Ni mbegu moja tu ya kiume ambayo hutumika kupatana na yai la mwanamke, japo huwa tunakosa kuamini hili kwani wakati mwingine ni vigumu mbegu hio kufikia yai la mwanamke.
Ukweli ni kwamba ukiwa na mbegu kibao utakuwa uwezekano huwa juu zaidi.
Acha kwa makini tucheki swala hili la uchache wa mbegu za kiume, chanzo chake, jinsi ya kujua kama una mbegu kidogo na njia za kushughulikia jambo hili
Ni nini maana ya kuwa na mbegu chache za kiume?
Kuwa na mbegu kidogo kunamaanisha kuwa maji maji ya kuweka mbegu yana mbegu chache.
Kwa swala la idadi, inammanisha kuwa mtu ana mbegu chini ya milioni kumi na tano kwa milimita moja ya maji maji ya kueka mbegu hizi. Huenda milioni kumi na tano ikawa ni nyingi sana lakini kulingana na utafiti mbegu milioni sabini na tano kwa milimita kumi na tano ya maji maji ya kuweka mbegu hizo ni kidogo sana
Ni nini husababisha uchache wa mbegu?
Sababu hizi ni:
Kunenepa kupita kiasai
Kuumia kwa makende ikiwemo kutokana na upasuaji
Shida ya kiafya kama ugonjwa wa kufura mishipa ya kifuko cha makende /pumbu
Hali ya kuzaliwa nayo/maumbile –Nam uchache wa mbegu za kiume huweza kuwa swala ulilozaliwa nalo.
Nitajuaje nina shida ya uchache wa mbegu za kiume?
Ishara kuu ni kukosa kuzalisha ama kutu. La kutia hofu ni huend kusiwe na ishara nyingine yoyote iliyo wazi.
Sasa nitahakikishaje nina shida hii?
Kufanyiwa uchunguzi wa majimaji yanayobeba mbegu za kiume.
Kufanyiwa uchunguzi katika mahabara husaidia kucheki kama mbegu za kiume zinafanya kazi ama la. Uchungu huu hufanywa angalau mara mbili ili kugundua shida. Lisikutatize akili, hii inafanyika kwa kutoa mbegu hizo kwa kujipuli kisha kumwaga kwa kikombe kisha zinapimwa.
Kando na kuangalia idadi ya mbegu,pia uchunguzi huu huangilia mahali mbegu zinakaa,wingi wake, uwezo kutembea kwake kwa sehemu za siri , muundo wake na jinsi zinafaa kufanya kazi
Ikiwa umepata matokea sasa,utafanyake?.
Ikiwa una mbegu chache ama huna kabisa, usitie hofu, kwani haimaanishi hutazalisha kabisa bali : uchunguzi zaidi utahitajika.Ikiwa huna mbegu kabisa, ongea na daktari ikiwa kuna matibabu zaidi.
Ukweli ni kwamba ukiwa na mbegu za kiume chache unaweza kukosa kupeana mimba.Hata hivyo ukiwa na mbegu chache bado waeza pata mtoto.
Je una swali lolote ama unataka kutoa maoni yako? Basi nena nasi kwa sehemu ya maoni yako
Mm ninashinda. Mmefura mshipa vle umesema. Cjui ntapataje usaidiz