Nini husababisha mbegu kidogo za kiume?
Inachukua mbegu moja ya kiume kuzalisha yai moja. Lakini hatufahamu kauli kuwa inaweza kuwa ngumu kwa mbegu hiyo kufika katika eneo la yai. Ukweli ni kuwa kiwango kikubwa cha mbegu ulizo nazo zina nafasi kubwa ya kuzalisha.
Hebu tuangalie kwa makini maana ya idadi ndogo ya mbegu za kiume, nini kinachosababisha nguvu kidogo za kiume na ni kitu gani unaweza kufanya.
Je inamaanisha nini kuwa na mbegu chache za kiume?
Kuwa na nguvu chache za kiume inamanisha kuwa una mbegu chache kupita kiwango cha kawaida.
Kwa idadi inamaanisha kuwa una chini ya mbegu 15M kwa mililita moja ya mbegu. Lakini mbegu 15M inaweza kuonekana kuwa nyingi sana. Ndio, milioni kumi na tano zenyewe. Lakini ikilinganishwa na kiwango cha kawaida cha milioni 75 kwa mililita moja milioni 15 ni ndogo mno.
Je nini kinachosababisha mbegu chache za kiume?
Baadhi ya sababu hizo ni:
- Uzito/kuwa mnene kupita kiasi.
- Shida katika pumbu/makende kama vile upasuaji.
- Baadhi ya hali za matibabu kama zile za msongo wa mawazo na msukumuo wa damu
- Pumbu kuwekwa kwa joto lisilo la kawaida
- Hali mbali mbali za kimatibabu kama vile Varicoceles,
- Uumbwaji wa viungo –Ni kweli kuwa mtu huenda akazaliwa na mbegu chache yani hali ya kimaumbile
Je nitajuaje nina mbegu chache za kiume?
Alama kubwa inayojulikana ni kutokuwa na uwezo wa kuwa na mtoto –au kutokuwa na uwezo wa kuzalisha au kuweka mtu mimba, kwa bahati mbaya kunaweza kukosekana dalili zingine
Je nitajuaje kama nina shida hii?
Jibu: Kupitia utathmini wa mbegu za kiume.
Utathmini wa mbegu za kiume unahusisha kupimwa katika maabara ambako kunakusaidia kuonyesha viwango vya usalishaji wa mbegu na kama mbegu hizo zinazalisha. Mara nyingi vipimo hivyo kufanywa angalau mara mbili iwapo idadi ya mbegu si za kawaida. Na pengine unashangaa mbegu huchukuliwa wakati unaambiwa ujifanyie punyeto kwa kikombe.
Zaidi ya hayo idadi ya mbegu, utathmini huo wa kimatibabu pia unaweza kuangazia mbegu ambayo inasaidia au hata kuathiri; wakati wa kuzaa, kiwango cha mbegu, idadi, wingi ama uchache wa mbegu, usafiri wa mbegu au mfumo wa mbegu.
Majibu yametoka sasa kipi kingine?
Mbali na majibu hayo kuonyesha idadi ndogo ya mbegu au hata kukosekana kwa mbegu haimaanishi kuwa hauna uwezo wa kuzalisha. Vipimo vya baadaye ni lazima vifanywe. Hata kama hakuna mbegu zimeonekana wakati wa uchunguzi wa maji maji ya uume, ongea na daktari wako kuhusu matibabu ambayo mbinu mbali mbali.
Hata hivyo ukweli ni kuwa kuwa na idadi ndogo ya mbegu inapunguza nafasi ya mbegu yako kuzalisha yai ambayo husababisha kupata mimba. Hata hivyo inawezekana kwa mwanamume mwenye idadi ndogo ya mbegu kupata mtoto.
Je una maswali au unataka kuongea nasi kuhusu ufahamu wako. Ongea nasi katika sehemu ya maoni