African american woman with braids holding birth control pills pointing finger to one

Ukweli kuhusu mbinu za kupanga uzazi za dharura

Vidonge vya dharura/E-pills, ambazo pia zinaitwa Asubuhi baada ya shughli/morning after ama mbinu za dharura zakuzuia mimba ni dawa ambazo unaeza tumia kama mumekulana  bila kinga kuzui kuzuia boll.

Vidonge vya dharura/E-pills, ambazo pia zinaitwa Asubuhi baada ya shughli/morning after ama mbinu za dharura zakuzuia mimba ni dawa ambazo unaeza tumia kama mumekulana  bila kinga kuzui kuzuia boll.

Unafaa kuzimeza muda huo huo baada ya kudinywa bila kinga, ndani ya siku 5 au masaa 120. Huo mda ukipita hazitakufaa au kukusort. Hizi E-pill zinapatikana katika maduka mob ya dawa ikimaanisha unaeza fika pharmacy bila kuuliza ushauri wa daktari.

Inaeza  kuwa jambo la busara uwe hivi vidonge/E-pills nyumbani iwapo utahitaji kuitumia. Basi hautakuwa na haja ya kukimbilia duka la dawa iwapo una dharura.

Kuna aina mbili za vidonge vya dharura vya kupanga uzazi, hata hivyo moja pekee ndio inapataika humu nchini Kenya. Ile inapatikana ni ile ya progestogen pekee (ambayo inatumia levanogestrel) mara nyingi huitwa P2.

Aina nyingine ya vidonge vya dharura ni ile ya IUD ya shaba. Hata hivyo nii huingizwa na mtaalamu wa matibabu.

Msee hakuna kiwango maalum cha kusema ni mara ngapi unaeza tumia dawa hizi kwa mwaka. Hata hivyo hii E-pill ina athari ya muda mchache. Hivyo basi, inaamanisha kuwa haifai kutumiwa kama mbinu ya kupanga uzazi ya kawaida ila tu wakati wa dharura.

Faida

Inasaidia kuzuia boll wakati mbinu ya kupanga uzazi imefeli au imesahaulika au wakati umebakwa.

Inamfanya mtu anakuwa na utulivu wa akili

Inapatikana kwa urahisi

Hasara

Inaeza kubadilisha mfumo wa kunyesha kwa mwanake( kuchelewesha au ikakuja mapema.)

Haiezi zuia magonjwa ya zinaa

Inafaa kucmezwa mara tu mtu anapofanya ngono bila kinga

Je hii E-pill ni sawa na kidonge cha kutoa mimba

E-pill sio sawa na vidonge vya uavyaji wa boli. Vidonge vya E-pill hufanya kazi kwa njia tofauti. Lakini haviezi fanya chochote kama yai tayari limetungishwa..

Kama tayari una boll na umeze hiki kidonge hakitaathiri boli yako.

did you find this useful?

Tell us what you think

LoveMatters Africa

Blush-free facts and stories about love, sex, and relationships