Je mfumo wa kutoa mjulus kabla kumwaga ni dhabiti?
Njia hii inataka mtu awe chonjo na timing yake na pengine uwe na bahati chungu nzima.
Kutoa mjulus kabla kumwaga inamaanisha kutoa uume kutoka kwa tupu ya mke kabla ya kumwaga.
Ni mbinu ya kudhibiti uzazi ambayo inazuia mshusho kuingia katika tupu ya mbele ya mwanamke.. Mwanamume anatoa mjulus wake kutoka kwa tupu ya mbele ya mwanamke na mbali na uke wa mwanamke kabla ya kumwaga.
Mfumo huo pia huitwa “ pull out” au pia “coitus interuptus” ikiwa unapenda maneno matamu kama hayo.
Je una namna gani?
Iwapo hauko tayari kuwa mumama au mubaba usitumie hii mbinu ya kutoa kabla kumwaga. Huwa sio mbinu poa ya kupanga uzazi. Kiwango chake cha kukufeli ni takriban asilimia 20 wakati unapoitumia pasi na umakini mwingi wakati wa ngono na asilimia 4 pekee ya ukiitumia kwa umakini mwingi.
Mbinu hiyo inahitaji kujizuia mwenyewe. Na sisemi kuwa usiwe na moja lakini je unayo.
Jamaa tuseme tu ukweli. Si rahisi kuitoa mjulus kwa wakati bana.
Wanaume wengi huhisi kama wako mbinguni na kukosa kuutoa mjulus kabla ya wakati.
Pili wanaume wengi huachilia mshusho kabla ya kumwaga kwenyewe. Iwapo maji maji ambayo hutoka kabla ya kumwaga yanabeba spamu basi ubora wa mbinu hii unapungua sana manzee. So kama unataka kutoa mjulus kabla umwage uwezekano wa kupata boli wa juu mno.
Kumbuka mamilioni ya spamu hutolewa lakini moja tu ndio inazalisha yai manzee.
Iwapo unalazima ya kutumia mbinu hii:
Hakikisha umetoa mjulus kwa wakati unaofaa. Ikiwa jamaa anakaribia kumwaga basi ni lazima atoe mjulus wake na ahakikishe kuwa anamwaga nje ya uke wa mwanamke.
Iwapo pia unataka cha pili, tatu au hata cha saba, basi mwanamume anahitaji kukojoa na kusafisha ncha ya uume. Hii itasaidia kuto spamu kutoka kwa mshusho.
Na kama kutoa mjulus hakukufanywa kwa wakati mzuri na unahofu kuwa utapataboll jaribu kutafuta mbinu za kuzuia boli za dharura.
Usisahau hili:
Mbinu hii haiezi kukukinga kutokana na magonjwa ya zinaa. Kwahivyo wakati wowote unafaa kutumia kinga kama kutumia mpira wa kondomu. Haya magojwa hayaendi manzee. Unaeza pata haya magonjwa wakati wowote unado sex ambayo si salama ama usipotumia kinga.
Masuala yanayolingana. Ukweli kuhusu mbinu za kutoa mjulus kabla ya kumwaga.
Je umejaribu hii mbinu msee?. Ilikuendeaje?. Ongea nasi katika sehemu yetu ya comments…