Je, ni kawaida kunyesha kusiko kwa kawaida kama unatumia Implant?
Hivi majuzi Halima aligundua kuwa hedhi yake sio ya kawaida. Hii kwake ilikuwa challenge kwa kuwa alikuwa mara nyingi yuko kwa hedhi kikawaida. Ana hisia tofauti na kushangaa ikiwa kifaa hicho kilichopachikwa hivi juzi kinaweza kuwa kinamsababisha madhara hayo.
Implant ni kifaa kidogo cha kupachikwa mwilini na ambacho hupachikwa juu ya bega mkononi na kutoa homoni aina ya progestin ambayo huzuia mimba. Ni njia mwafaka ya kutumia ambayo inaweza kutumika kuzuia kizazi.
Wengine wanaotumia vidonge vya kupachika wanaweza kupata hali zisizo za kawaida za kutoa damu za hedhi ama mabadiliko ya wakati na uzito wa hedhi. Wanawake wengine wanaeza pata hedhi nyepesi, huku wengine wanaweza pata ongezeko la damu katikati ya hedhi. Hii huwa ni ya muda tu kwa sababu mwili huwa unaenda ukizoea mabadiliko ya kifaa hicho ulicho kiweka kwa mwiili.
Athari nyingine za kuweka kifaa mwilini ni kuugua kwa maumivu ya damu ya hedhi nakuongezeka kwa hedhi wengine wanaotumia wanaweza kuwa na matone ya damu ya muda au pia kuanza kunyesha kusiko kwa kawaida.
Ni muhimu kutaja kuwa kila mmoja hawezi kuwa na mabadiliko ya damu ya hedhi.
Kumbuka unapopata mabadiliko ya kila mara ya hedhi ukiwa unatumia kidonge unashauriwa kutafuata ushauri kutoka kwa mhudumu wako wa afya .wanaweza kutathmini iwapo kidonge hicho kinakufaa na pia watakushauri jinsi ya kujikinga na madhara au hata kukupa ushauri wa kimatibabu.
Ili kutilia mkazo hedhi ilichukua muda mrefu inafaa kukutoa wasiwasi kwa kuwa inaweza kuwa inasababisha wana mambo mengi nasio hicho kifaa cha kupachika.