Mbona ngozi yangu katika sehemu nyeti ni nyeusi mno yatofautiana na sehemu zingine za mwili?
Najuwa wengi wamelitambua hili la rangi iliyopasha mno katika sehemu zetu za siri. Ndio au la? Sababu ya utafauti huo ni kuwa ngozi ilioko katika sehemu nyeti na maeneo yake huwa laini kutokana na MELANINI.Melanini ni tukio la kimaumbile ambalo udhibiti uwezo wa ngozi,macho na nywele kubadilika rangi.
Ngozi ilioko katika sehemu nyeti na maeneo hayo hii tukijumulisha mashavu/mdomo wa kuma, SCROTRUM/korodani na mkundu. hizi sehemu huwa na rangi yakupasha mno kuliko zile zingine mwilini.Inakuwa hivyo kwa kuwepo kwa idadi nyingi ya chembechembe ya melanini inayozalishwa na si kama kwengine mwilini.
Kwa hivyo hili ni jambo la kawaida lisilotaka wasiwasi tunapoziona sehemu zetu nyeti na maeneo yake kuwa na rangi ya kupasha sanasana nyeusi.Hili ni tendo la maumbile ya miili yetu.Mwisho wa kwisha ,litokapo badiliko linaokupa wasiwasi ni bora utafute ushauri kutoka kwa dakitari au mtaalamu.Ukifanya hivi,kila swali lako litapata jibu sahihi mwishowe uishi vyema bila wasiwasi.
Kublichi/kujichibua maeneo ya sehemu nyeti:
Si jambo la salama na madhara yake ni mabaya kwa wanaoblichi sehemu hizi.Lako la msingi ni kuzingatia usafi kwa ubora wake.Hilo la kubadili rangi yako kwa umarufu kublichi tafakari. La msingi ni kutafuta ushauri nasaha kwa wataalamu wenye hizo taaluma.
Je umewahi jiuliza mbona sehemu nyeti na maeneo yake huwa na rangi ya kupasha mno kuliko sehemu zingine za mwili?