woman covers the nose with hand

Mbona damu hutoa harufu ya chuma wakati wa hedhi?

Wakati ni wa hedhi/kuvuja, uko pale ukibadilisha padi/sodo, tamponi au menstrual cup unapigwa na harufu tatanishi kutoka katika sehemu zako nyeti . Ni harufu ambayo umeizoea  baadaye unaskia ikinuka kama chuma .la kushangaza,wewe mwenyewe ni mtu safi na mnuko huo wa damu unakupa tumbo joto na wasiwasi.

Wakati ni wa hedhi/kuvuja, uko pale ukibadilisha padi/sodo, tamponi au menstrual cup unapigwa na harufu tatanishi kutoka katika sehemu zako nyeti . Ni harufu ambayo umeizoea  baadaye unaskia ikinuka kama chuma .la kushangaza,wewe mwenyewe ni mtu safi na mnuko huo wa damu unakupa tumbo joto na wasiwasi.

Kupata hedhi ni jambo la kawaida kwa mwanamke aliyevunja ungo, na ni kawaida ya damu hiyo kutoa au kuwa na harufu. Pia ujuwe fika kuwa, kila mwanamke huwa na harufu yake na wengi wao harufu huwa mbaya na ya kukera na hutambulica kama harufu ya chuma.

Tunataka kuwajuza kuwa licha ya harufu hiyo mbaya, tutoe shaka kama wanawake kwasababu ni jambo la kawaida, ila harufu haifai kuendelea zaidi baadai ya siku zako za hedhi.

Harufu ya damu wakati wa hedhi ni kutokana na uwepo wa (iron/chuma) kiungo muhimu ambacho ni mojawapo kwa (hemoglobin) virutubishi vinavyobeba hewa safi(oxygen). Hiyo damu inapotoka na kuchanganyika na hewa hapo ndipo huanza kupata harufu hiyo ya chuma. Tutilie maanani uke wa mwanamke huwa na harufu yake, basi zikichanganyika zote, harufu inakuwa ni ya chuma ama kutu.

Je nawezaje kuistamili hii harufu?

Kama wewe ndio muhusika, yafaa uliweke akilini kuwa harufu hiyo  ya damu wakati wa hedhi ni yako na haitambuliwi au kunukia watu wengine. Kuwa safi/nadhifu wakati huo wa hedhi ndio suluhu maanake ukijiweka safi huwa unapunguza harufu hiyo na kudhibiti maonekano yako na sehemu zako nyeti.

Usafi wakuzingatiwa ni ule wa; ubadilishaji wa padi/sodo, tamponi ulizotumia, kuosha sehemu hiyo kwa maji mengi na sabuni laini. Onyo kwa wale wakutumia bidhaa za kemikali kali kali.Hizi kemikali huhatarisha ubora wa afya ya sehemu yako nyeti.

Kwa kujumuisha, twalijuwa hilo la harufu ya damu wakati wa Hedhi ni la kawaida. Tusipuuze mabadiliko ya harufu na ikifwatiwa na ishara tatanishi. Kuna haja ya kumtembelea mtaalamu wa afya kwa ushauri na nasaha kuhusu usafi wote wa afya ya uzazi na ustawi.

did you find this useful?

Tell us what you think

LoveMatters Africa

Blush-free facts and stories about love, sex, and relationships