banana with white thick fluid dripping

Je, rangi ya shawawa/shahawa ni gani?

Tukianza na wewe, je shahawa/ yako ni rangi gani kwa sasa?.wengi uliekea hili mapuuza na kushughulikia  mambo mengine ya kimaisha. Hili pia ni La msingi kuzingatiwa na kupewa kipaumbele katika maswala yako ya  afiya.wale hawaja tilia maanani kujuwa, basi lijuweni ndiposa utaelewa ni rangi gani ni ya kawaida na ipi ya kutilia shaka.

Utaalamu umedhibitisha kuwa rangi ya kawaida na iliyo ya sawa kwa SHAHAWA ni nyeupe nyepesi, hadi ya kijivu ambayo haijapasha,si kwa sana pia huwa na umanjano kwa mbali.Huu mchipuko inakadiriwa kuwa sawa na uchangizwa sana na; uzito za uzalishaji wa SHAHAWA kwa mwili,ni mara ngapi mtu humwaga (EJACULATE), lishe ya mtu na mtindo wa kimaisha kujumuisha afya ya mtu.

SHAHAWA inajumuisha vitu kama spermatozoa, fructose, enzymes na proteini.Yote haya huchangiya kwa mtazamo wa rangi.Kama tulivyoeleza awali,rangi iwe ni nyeupe nyeupe, au kijivu jivu , au majano nyepesi kwa mbali.

Makadirio ya kumwaya (ejaculation) pia inaweza kuathiri pakubwa rangi ya  SHAHAWA.Shahawai iliyo ifadhiwa kwa vibeseni vya SHAHAWA kwa mda mrefu, kwa mtazamo huenekana kuwa na rangi ya manjano isiyo pasha tofauti na mshusho  mpya.Pia, lishe  na mitindo ya chakula kadhaa au virutubishi. Uraibu wa pombe na uvutaji sigara pia uchangia mabadiliko ya rangi ya mshusho lakini hili si kwa sana vile.

Kuwepo na uwekaji mzuri wa maji{hydration} ina umuhimu kwa kubadilisha rangi ya mshusho na kuithibiti.Kuwepo kwa usambazaji wa maji inaweza kusababisha mshusho uonekane ukiwa umepasha na kupata rangi ya kuiva.Kwa ubora wake inafaa mtu adhibiti sana unywaji wake wa maji kwa kila hatua kwa manufaa ya kustawisha rangi na ubora wa mshusho.

Hatuwezi kupinga utofauti wa rangi ya mshusho kwa jumla, pia tuzingatie kuwa, mabaliko ya rangi yanaisharia kuwepo kwa dalili za maradhi au changamoto na upungufu .Kwa mfano muonekano wa  damu kwa mshusho (hamatospermia) kukiwa hivyo basi kuna uwezekano wa rangi ya zambarau/pinki au uwekundu fulani, ikifikia hapo basi muhusika anahitajika kufanyiwa utafiti wa kina.Pia kuwepo kwa rangi ya kijani jani na harufu mbaya ya mshusho ni ishara ya uambukizaji na pia lataka uchunguzi na muhudumu wa afya.

Kwa kujumuisha,rangi ya kawaida ya mshusho ni nyeupe, na yakijivu jivu nyepesi na manjano kwa mbali, utofauti kuambatana na rangi hizo inaeza kuwa ni sawa.lakini ukiona utafauti mwingine unaozidi basi huna budi kuhusisha muhudumu wa afya kuliweka sawa uwezekano  umepata dharura ya ugonjwa/maambukizi na matibabu .

Tafadhali pata ushauri kwa dakitari unapoona mabadiliko kwa rangi yako ya mshusho.

did you find this useful?

Tell us what you think

LoveMatters Africa

Blush-free facts and stories about love, sex, and relationships