Niko na boli. Je nifanyeje?
Ukifanya ngono bila kinga we juwa tu kuna uwezekano boli itaingia. So, ukipata hiyo mimba utafanyaje?
Na wale wako mpangoni wa kupata mimba twawapa kongole! Elekea kwa sehemu inayoeleza maswala ya ujauzito utapata maelezo kibao kuhusu unaloyatarajia.
Wadau wengi kupata boli inakujia kama jambo la kushangaza.Na ni rahisi sana kujisahau na hata kutotumia mpira/kondomu utamu ukinogea.Na pia si wakati wote ukitumia njia za kupanga uzazi huwa zinaenda tunavyotaka.
Na likitokea lakutokea upate boli muhimu ni kuweza kufanya uamuzi ya nilipi utafanya.
Kuna mapendekezo matatu
- Unaeza kubaki na mtoi
- kuna kuzaa mtoi halafu unapeana kwa ukubaji/adoption ama kumpa mmoja wa familia yako.
- Mwisho wa kwisha unaeza kutoa boli.
Wewe kile utakacho amua, kuna na kuwaza kuhusu litakalo fuata mbeleni. Bonga na mtu unaemweka karibu na mwenye busara ya kukupa na mwisho wa kwisha wa kukuinua ; huyu bila shaka anaeza kuwa ; mama, baba, rafiki , shangazi,mshambulizi wako au hata muhudumu wa afya .yule hawezi kukubaguwa kwa uamuzi wako. Mwisho wa kwisha ni wewe wakuamua.
Siku zote ongea na yule unaemuamini. Ukiwa na uhakika wa uamuzi wako, utajihisi poa baadaye. Yote tisa kumi, uamuzi utoke kwako na uwe wa heri. Wachana na presha za watu wengine na ikiwa haufil poa na ushawishi wao ,cheza mbali nao.
Baki na mtoto
Unaeza kuamua kubaki na mwanao,hii itamaanisha uanze kufikiria maisha ya mbele:
- piga bongo kuhusu ni vipi utaweka mikakati ya vile utajikimu na mtoi ambae anakutegemea?
- Jiulize, je kuna uwepo wa mpango na msaada kutoka kwa babake mtoto,kuungwa mkono na jamii yako au ya baba mtoto.?
- Je itaathiri vipi Mipango yako ya sasa ,kesho na siku zijazo ukizingatia maisha yako?
- Je kuhusu masomo ama mipangilio ya kazi?
- Je utapata msaada kutoka kwa babake motto au familia yako?
- Je una rasilimali zakusitiri kimaisha?
- Kama una mpenzi ,mawazo yake ni yepi?.
- Je anataka mumueke mtoto?
- Je watoto una watoto wangapi tayari?
- Je wataka motto mwengine?
- Mwanao tumboni ako shwari?
- Wewe uko fureshi ki afya?
- Mwisho wa kwisha mamake , swali muhimu ni je wamtaka huyu mtoto?
Peana mtoto kwa ukubaji/adoption
Unaeza mpeana mtoto ukishamzaa kwa ukubaji au adoption. Hili lataka bongo sana na kuangalia uchaguzi ulio nao. Ukiamua kuchukua huu uamuzi, basi itakubidi kujiuliza, nani atakaye mchukua motto wako?
Unaweza kuwasakanya watu wa shughuli hizi nao watakupa mipangilio na sheria ya jinsi mtoto wako ataadoptiwa kupitia taratibu za kitaifa na mwisho wa kwisha lazima upige sahihi ya ukubaliano na vile utawafikishia motto mara tu unapomzaa. Mara nyengi mashirika yanayoshighulikia swala hili hukupendekezea kumwacha motto pale hospitalini alipozaliwa ili waweze kumchukua.
Kwa wale ambao bado wanaishi na wazazi wao ,ni poa ukiwa wazi na wazazi wako. Ukiwa kijana hujawa mtu mzima huwa una uchache wa uchaguzi. Wazazi wako wanaweza kutaka kukusaidia kumlea mtoto, . Ukiwa na ugumu wakuwaeleza basi rafiki yako aa mmoja wa familia yako anweza kuwapa habari hizi.
Wachana na mambo ya kuamua kumwacha mtoto ama kumtupa. Ni bora zaidi kumuacha hosipitalini,kanisani, ama na shirika linalowaadopt iliwalindwe na kukuzwa.
Kutoa mimba
Uchaguzi wa tatu ni kuitoa mimba. Ijulikane kuwa kama uamuzi mwengine wowote huu uamuzi si jambo rahisi na unahitaji mda wa kutosha upige bongo juu ya jambo hilo. La muhimu ni wewe ujiamulie kwasababu hili lina kuusu wewe, mwili wako na uamuzi wako. Soma Zaidi kuhusuaina tofauti za kuavya ama kutoa mimba.
Uamuzi wako
Hakuna jibu sahihi au lisilokuwa sahihi, ukisema na kuamua ni hivyo, bora limetoka kwako. Zaidi ya yote liwe lile waliona ni la kheri kwako. Ukiwa na ugumu wa kufanya uamuzi unaweza muhusisha mtu wako wa karibu unayemwamini.
Yakitoka nje, basi kuna hosipitali zakufahamika kwa shughuli za kuavya/kutoa mimba,tia guu lako huko upate mawili matatu na ushauri utakaokusaidia kufanya uamuzi.