sad woman staring at a pregnancy test

Je kuosha kuma baada ya ngono je kunaeza zuia boll?

Baada ya ngono ambayo haina kinga Doreen alianza kuogopa kuhusu kupata boll. Ili kuzia boll aliosha kuma yake mara mbili kwa siku kwa wiki tatu mfululizo baada ya kushauriwa na beshte yake Mwende. Huu haukuwa ushauri poa juu kuma yake haiku feel poa.

Baadaye alianza kuathirika kizazi yake hali iliyomlazimisha kutembelea kiutembelea daktari.

Kuna dhana mbovu kuwa kuiosha vagina ni njia poa ya kuzuia mimba.

Mimba hutokea kama sperms za mwanamume zimegusa mayai ya dem  hayakufanyika katikati mpira wa kizazi na kusaisha kuma hakuezi kuzuia sperms kufikia yai.

Kutumia vifaa mbaya za kusafisha kama vile sabuni ya marashi kusafisha kuma inaeza zuia hali yake ya unyevunyevu na hata kupata baktiria. Hii inaeza kusababisha mwasho maradhi na hata masuala mengine ya kiafya.

Ni muhimu kukumbuka kuwa njia mwafaka ya kuzuia boll baada ya sex nikutumia vifaa vya kuzuia mimba hasa vifaa za dharura vya kuzuia mimba, dawa za kumeza ili kuzuia mimba na vifaa vya kujiingiza kwa mwili . Kila njia ya kuzuia mimba ina maelezo maalum ambayo yanafaa kuzingatiwa ili kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Dawa inayofahamika kama morning pill ndio njia inayotumika zaidi kuzuia mimba yenye kinga.

Ni muhimu kujieleimisha kuhusu mbinu bora za kujikinga na pia kutafuta ushauri wa daktari ili kufahamu ni mbinu bora inayoambatana na afya yako, upendayo na kulingana na wakati.

Kufanya maamuzi yafaayo na kutumia mbinu bora mara kwa mara ni njia nzuri ya kujikinga na mimba isiyotarajiwa.

Kwako tena je ni mbinu gani ambazo umezitumia kuzuiamimba. Ongea nasi katika sehemu ya maoni.

did you find this useful?

Tell us what you think

LoveMatters Africa

Blush-free facts and stories about love, sex, and relationships