scared man in mustard t-short

Je, niache kufanya ngono nikiwa na gonjwa la zinaa?

Umepokea majibu kuwa una gonjwa la zinaa. Mawazo kibao yanakusonga, na wajiuliza kama uwache kupiga ngoma ama vipi?

Magonjwa ya zinaa ni jambo la kawaida , na huenda wengi wetu wakayapata maishani. Hata kama ngono ndiyo njia kuu yakusambaza haya magonjwa, kuna njia nyengine kibao zakusambaza haya magojwa kama kugusana kwa ngozi, ama mama kumuambukiza mwanawe  akiwa mjamzito, akinyonyesha ama wakati akizaa.

Tuelewe freshi kuwa ngono ndio njia kuu yakusambaza haya magonjwa ya zinaa.

Je, tuwache kuchapana tukiwa na gonjwa la zinaa?

Wewe na mwenzako mnaye shikiri naye ngono mkipimwa mupatikane na gonjwa la zinaa, inaweza kuwabidi kusitisha kufanya ngono. Ijapokuwa matumizi sawa ya mipira ya kondomu yanapunguza pakubwa uwezekano wa kupata haya magonjwa, bado kuna uwezekano yakupata ama kumsambazia mwenzako gonjwa la zina kwasababu mipira ya kondomu haizuii kwa asilimia mia moja.

Isitoshe , gonjwa la zinaa haliathiri tu sehemu za siri lakini pia linaathiri kinywa na rektamu pia. Hii inamaanisha tusijihusishe kwa ngono ya mdomo ama tupu ya nyuma.

Basi baada ya kujua hali yako , inapendekezwa uchukuwe madawa na kuyameza kama alivyoagiza daktari, usiwache kumeza kwa sababu dalili zimepotea ama kwasababu wajiskia vyema .

Ukilazimika…

Ikikubidi kufanya ngono hasa kama una gonjwa la zinaa ambalo linaweza kutibika kwa urahisi kama Klamidia, na uko kwa matibabu, endelea kutumia mipira ya kondomu kwa ngono ya kuma na tupu ya nyuma, na mipira yenye ladha na mabawa ya meno kwa ngono isiyo yakuingiliana. Unapaswa kuendelea mpaka mhudumu wako wa afya aseme umetibiwa na kuwa unaweza kufanya ngono bila kinga. Hadi huwo wakati basi hakikisha unafanya mapenzi bila kinga.

Ukiwa na gonjwa lazinaa lisilotibika kama malengelenge,VVU,(virusi vinavyosababisha ukimwi) na vidonda vya uzazi, usijihusishe kwa tendo la ngono na wengine hadi umalize dawa zako na mwili wako kuwa katika  hali ambayo virusi vinavyosababisha ukimwi mwilini mwako havionekani kwa damu yako. Ikiwa hii ndio hali basi wachana na kufanya ngono ya kujikinga.

Kumbuka!

Inapendekezwa uwajulisha watu uliofanya nao ngono ili nao pia wakapimwe. Hili laweza kukutatiza kimawazo lakini ni jambo la sawa kwasababu afya yao imo hatarini.

Je, uko na swali lolote au changizi ungependea kusimulia? Tuongeleshe katika sehemu ya mapendekezo.

did you find this useful?

Tell us what you think

LoveMatters Africa

Blush-free facts and stories about love, sex, and relationships