Je, ni madhara gani yanayoweza kutokea kwa kutumia PrEP?
Sam, jamaa anaefanya kazi benki mwenye umri wa miaka 38, alipata madhara baada ya kutumia PrEP ambayo yalimfanya kutaka kuacha kutumia dawa hizo. Salome, msaidizi wa kibinafsi, alipata athari, ila kwa muda mfupi. Kila mtu ana uzoefu wa kipekee anapotumia Pre-exposure prophylaxis (PrEP).
PrEP ni njia bora ya kuzuia virusi vya ukimwi, lakini kama dawa yoyote ile, inaweza kuwa na madhara. Ila kwa ujumla madhara yake ni madogo na ya muda. Athari hizi mara nyingi hupungua kadiri mwili unavyozoea dawa.
Madhara ya kawaida ya PrEP ni pamoja na:
1. Kichefuchefu(kusikia kutapika)
2. Maumivu ya kichwa
3. Usumbufu ndani ya matumbo
Dalili hizi kwa kawaida ni za muda na zinaweza kupotea ndani ya wiki chache baada ya kuanza kutumia dawa za PrEP. Watu wengine wanaweza kupata mabadiliko kwenye matumizi ya figo. Ufuatiliaji wa huduma za afya mara kwa mara ni muhimu ili kujua matatizo yoyote yanayoweza kutokea mapema, na marekebisho ama mageuzi ya dawa yakafanywa panapokuwa na hoja.
Ni muhimu kutambua kwamba madhara makubwa ni nadra sana lakini yanaweza kusababisha matatizo makubwa ya figo au mifupa tunapotumia dawa hizi kwa muda murefu. Japokuwa hatari hizi ni za kutisha na kuogopesha, ni muhimu kuzipima hizi hatari dhidi ya faida kubwa zinazokuja na kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Yeyote anaetumia PrEP anapaswa kuwa na mawasiliano ya wazi na mtoaji huduma wake wa afya. Uchunguzi wa mara kwa mara hurusu ufuatiliaji na utambuaji wa madhara yanayoweza kutokea kwa kutumia dawa hizi na kuhakikisha kwamba watu wote wanapokea huduma na msaada inavyofaa.
Kwa ujumla, watu wengi wanaotumia PrEP hupata madhara madogo, lakini faida za kuzuia uambukizaji wa virusi vya ukimwi yanazidi kwa ukubwa na umbali hatari zinazoweza kutokea kwa watu wengi