A blue PREP tablet on a palm

Je, naeza kuambukizwa Ukimwi nikiwa kwa PrEP?

Uzuiaji wa maambukizi ya virusi vya UKIMWI kabla ya kutiana (PrEP) umebadilisha sana kinga dhidi ya Virusi Vya Ukimwi/VVU kwa kupunguza sana hatari ya kuambukizwa virusi hivyo unapotumia mara kwa mara. Lakini, hii PrEP ni yenye ina uwezo kiasi gani?

PrEP hupunguza nafasi ya kuambukizwa VVU kwa kuzuia virusi vya UKIMWI kuingia mwilini mtu anapokutana navyo. Kulingana na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), PrEP ni asilimia 99% yenye uwezo ikiwa inachukuliwa kama ilivyoelekezwa. Kwa wale wanajidunga/kujibwenga dawa za kulevya, PrEP ni angalau asilimia 74% yenye uwezo. Kwa sababu ya ulinzi huu, PrEP ni kitu muhimu sana katika kupambana na VVU, hasa kwa wale walio katika hatari ya kuambukizwa.

Inafaa ukumbuke poa kuwa hata na uwezo wake wa juu, PrEP haizuii asilimia 100% dhidi ya VVU. Kuna wakati mwengine japo nadra sana, ambapo watu wamepata VVU wakiwa kwenye PrEP. Hii inaweza kutokea kutokana na mambo kama vile kukosa dozi lako, mwingiliano wa dawa tofautitofauti, au kukutana na aina za VVU ambavyo vinahimili  dawa. Zaidi ya hayo, PrEP haizuii magonjwa mengine ya zinaa (STIs).

Kwa hiyo, ijapokuwa PrEP inapunguza sana hatari ya maambukizi ya VVU, ni muhimu kwa watu wanaotumia PrEP kuendelea kutumia njia salama za ngono, kama vile kutumia kondomu, na kufanyiwa vipimo vya mara kwa mara vya VVU na magonjwa mengine ya zinaa. Pia ni muhimu kwa wale wanaotoa huduma za afya kuwafuatilia watumiaji wa PrEP mara kwa mara ili kuhakikisha wanazingatia vizuri na kuwasaidia kukiwa na wasiwasi au athari yoyote.

Kwa kumalizia, itambulike kuwa ingawa PrEP ina uwezo mkubwa katika kuzuia maambukizi ya VVU, haizuii asilimia 100%. Hata hivyo, inapotumiwa kama mojawapo ya mpango mzima wa kuzuia VVU unao husisha vipimo vya mara kwa mara na njia salama za ngono, PrEP inaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya maambukizi ya VVU na kuchangia katika afya na ustawi wa kijinsia kwa ujumla.

did you find this useful?

Tell us what you think

LoveMatters Africa

Blush-free facts and stories about love, sex, and relationships