Njia za kuujali Ujauzito ukiwa na virusi vinavyo sababisha ukimwi
Ukiwa unaishi na virusi vya ukimwi na uboli juu, tena unataka kuanzisha jamii yako, nibora kuwa na uamakini sana kujikinga na mtoto wako aliye tumboni.
Kuna njia kibao unaweza kutumia kulinda boli yako na motto wako ukiwa unaishi na virusi vinavyosababisha ukimwi.
Kabla ya ujauzito/boli
Wewe ukiona mda ndio sasa, kuna vile wajisikia kupata motto lisikutie shaka kamwe tia guu lako kwa muhudumu akupe moja mbili za venye kutaenda na hali yako ya virusi. Kwa sana watasisitiza sana kumeza dawa zako ili uwe katika hali ambayo virusi vya ukimwi havionekani katika damu yako kabla kujzwa boli.Ukimtembelea mhudumu wa afya atakueleza kama wawweza kuendelea na matibabu yako ama kama itakulazimu kubadilisha ili usimwathiri motto aliye tumboni..
Kuenda kwako kwa muhudumu ni muhimu kwani kutakufundisha kuhusu jinsi virusi vinanasambazwa kutoka kwa mama hadi kwa motto wake akiwa mja mzito, na hasa umuhimu wa kumeza vidonge vyakokila sikukupunguza uwezekano huuo. Itakusaidia Zaidi kufanya uamuzi wakisawa.
Wakati wa ujauzito
Mimba yako ikkishahikikishwa na mmhudumu wa afya, omba mkutano na mhudumu amwenye ujuzi wa Virusi Vinavyosabisha ukimwi kubonga naye kuhusu jinsi utapunguza uwezekano wakusambaza virusi hivi kwa mwanao.
Nenda kama kliniki za kawaida, utapimwa virusi vyako na kiwango ukikijuwa ni hivyo utaishi salama na ya kinga kuimarika.kuna na wale umepata boli na hujui hali yako, ikifika hapo itabidi upimwe ,haswaa mambo na damu na kama vipi pia utaratibu wa madawa utapewa.
Safari yako ya kuwa na boli,ni kwenda kurudi kibao kwa watalamu w afya na kila ukipatia guu wewe bwabata kinachokukera kuhusiana na afya yako ya uzazi.
Mda wa kujifungua na tumbo kuita
hapa ndio macho yatakodolewa maanake kuna na uwezekano wa kuambukiza anayezaliwa kutoka kwa mamake virusi vya HIV.watkusorora uzito wa virusi vyako kwa damu na kama vipe watakupa la hoja au haja.haswa kujivungua kupitia kisu ikiwa ndio moja ya uhakika.
Kujitunza badae ukishajifungua
ukishajifungua si mwisho, mwana mchanga pia anapimwa ngoma. Si mwisho baada ya wiki 4 na 6 ngoma inapimwa tena.mengi ya kukutoa taka pia yazingatie.ukiambiwa ni kumyonyesha basi usiliache kwa ujuaji na kuchanganya na vya madukani.Hatari nikuchanganya vyakula kwa mwanetu mchanga ni kuipa nguvu hatari ya kunasa virusi kwake.mamake pindu umemalizana na kunyonyesha huyo mwana mchanga atapimwa tena virusi na watakupa lakukujenga kulingana na matokeo.
Na kama vipi ongeleshana na dakitari kuhusu kunyonya kwa mwanako na kama unaona kuna vile anaeza pata lishe kwa njia nyingine,litamke mamake.hili lina ubora wake maanake pia litamzuia kuambukiwa HIV.
Wewe pia husiache matibabu yako,meza ARV kama kawaida kujifungua isiwe sababu.litasaidia sana kupunguza makali ya ngoma kwenye damu yako.
Maagizo yote ya ujauzito utakayo pewa ,yafanyie akili kwa kuyaelewa vilivyo kwa afya yako na ya mwanao mchanga.vinatokea wewe kuwa na virusi na mwanao kukosa virusi hivyo tusipuuze.