Je, muda wa kuishi kwa mtu mwenye virusi vya ukimwi ni upi?
Jason, jamaa la pwani anaefanya kazi kwa banki na mwenye umri wa miaka thelathini aligundua ako na virusi vya ukimwi mwaka wa 2023. Amejitahidi kukubali hali yake na imekuwa vigumu sana kuishi kila siku. Mara nyingi huwa anajiuliza ana muda gani wa kuishi na mawazo ya kifo yanamfadhaisha sana.
Alipogunduliwa kwa mara ya kwanza katika kituo cha VCT huko Nyali, alihisi kama alikuwa amepewa kifungo cha kifo. Tangu wakati huo, amekosa usingizi, mara nyingi akiwa na wasiwasi ikiwa ataishi kutimiza ndoto zake. Ana maono ya kuendeleza elimu yake na kufanya kazi na banki kuu ya kimataifa siku moja.
Ikiwa unapitia hali anayopitia Jason, kuna tumaini. Urefu wa Maisha ya jamaa alie na virusi imeongezeka kwa kasi kwa hizi miaka zilizo pita, kutokana na maendeleo katika matibabu na utunzaji. Hapo mwanzoni mwa janga la ukimwi, matokeo ya kuwa na virusi mara nyingi yalimaanisha kupunguzwa kwa muda wa maisha ya mtu. Hata hivyo, pamoja na maendeleo ya tiba ya kurefusha maisha (ART), watu wanaoishi na virusi sasa wanaweza kutarajia kuishi maisha marefu na yenye kuridhisha.
Kulingana na utafiti wa sasa wa kiafya, mtu mwenye virusi na anayefuata utaratibu wa ART anaweza kuwa na umri wa kuishi sawa na wa mtu ambaye hana Virusi. Kwa matibabu sahihi na usimamizi mzuri wa virusi, watu binafsi wanaweza kudumisha afya njema na kupunguza hatari ya kusambaza ukimwi kwa wengine.
Mambo kama vile kujitambua mapema, kupata huduma ya kiafya, kuchukua dawa kama ilivyoagizwa, maamuzi ya maisha yako, na kuwepo kwa hali zingine za afya kunaweza kuathiri muda ambao mtu amwenye virusi anaenda kuishi.
Zaidi ya hayo, maendeleo katika sekta ya matibabu ya ukimwi yanaendelea kuboreka, kutoa njia mpwa za kudhibiti virusi kwa urahisi na yenye madhara chache.