Ninafaa kupimwa virusi vya ukimwi baada ya muda gani?
Mwanzo wa mwaka Michael alihofia kuwa angepata ukimwi kutoka kwa mwigizaji mmoja ambaye walikutana naye katika klabu siku za wikendi. Baada ya wiki mbili alienda kliniki na kupata vipimo. Daktari hata hivyo alimshauri kupata vipimo vingine baada ya muda wa kipindi cha mwanya.
Muda wa kipindi cha mwanya ni ule muda kati maambukizwa na muda wa virusi kuonekana kwa damu. Muda huo unategemea na aina ya kipimo kilichotumika. Kwa kipimo cha antigen / kingamwili kawaida muda huo huwa ni siku 18 hadi siku 90. Michael alishauriwa kupima tena baada ya siku 90 ili kupata majibu kamili.
Daktari alimwambia kusubiri ili kuvipa muda virusi kuongezeka/kuzaana na kuonekana kwa damu yake.
Kupima kwa wakati ni muhimu ili kujua iwapo umeathirika, au hata kuhakikisha unapata matibabu yafaayo na pia utulivu wa akili kwa wale ambao wanahisi huenda wakapata ukimwi.
Kutegemea kiwango chako cha hatari ya maambukizi daktari wako atakushauri iwapo utahitajika kutumia dawa za kuzuia ukimwi/ kuwekwa chini ya kinga kabla ya kuambukizwa (PrEP). Haya hapa ni mambo yote unayohitaji kuyafahamu.
Mbinu mbali mbali za kupima ukimwi zina muda tofauti tofauti:
- Vipimo vya kingamwili vya maabara- hii hufanywa na kiwango kidogo cha sampuli yad amu kutoka kwa mshipa-hufanya kati ya siku 18-45
- Vipimo vya asidi ya kiini (NAT) -unaonyesha hali ya kirusi – hufanywa kati ya siku 10 na siku 33
- Vipimo vya mahali pa huduma vinavyofanywa– hufanywa kwa kuingiza kifaa cha upimaji katika mdomo wa mgomjwa- hutumika kwa siku 90.
Upimaji unoafanywa nyumbani- una usiri napia ni mbinu bora. Pia inaruhusu kila mmoja kujipima mwenyewe kutumia sampuli za mate na damu. Upimaji huu hutoa majibu ndani ya dakika za kuhesabu. Hata hivyo inapendekekezwa kuthibitisha majibu kutoka kwa mtaalamu wa afya.
Upimaji wa nyumbani unaharakisha kutambuliwa kwa mapema. Kuchangia katika kudhibiti na jitihada za kuzuia. Ni muhimu kuangazia kuwa haimaanishi kuwa majibu yanayoonyesha kuwa huna ukimwi ni kwamba huna magonjwa mengine ya zinaa.
Upimaji wa kila mara unatarajiwa kupunguza athari ya kupatikana na magonjwa, unahakikisha usimamizi bora, hali inayochangia jitihada za kuzuia maambukizi na kuimarisha hali ya kiafya.
Kituo cha kuzuia magonjwa na CDC kinapendekeza kupimwa angalau mara moja kwa mwaka iwapo umejihusisha katika vitendo vinavyoweza kukuleta ugonjwa wa ukimwi.