a screen computer showing man and woman laying on each other

Je, ngono ya ponografia ni kweli?

Je, ni kila kitu unachokiona kwa ngono ya ponografia unafaa kukifanya kitandani? Je, umewahi kujaribu ujuzi ambao umeona wa video za ngono?. Je ilikuwaje? Inawezekana haikufanyika vizuri. Sio wewe peke yako.

Baadhi ya video za ngono zinafaa kuwa na ilani ya usijaribu hii ukiwa nyumbani. Maana mambo tunayoyaona waa!.

Kutoka kwa mboro kubwa kubwa. Ngono inayoendelea kwa muda mrefu. Style za akrobati na wahusika ambao huwa washusha mara nyingi na miili yenye viungo vya kuvutia na ambayo imelainishwa. Ngono za video zinaweza kukufanya ukahisi kwamba unakasoro

Unashangaa umekuwa na wapenzi wengi na haujakutana na mwenye ujuzi mwingi wa masuala ya ngono. Unafaa kukaa chini na kutafakari kwa sababu pia wewe hauna ujuzi kama huo.

Kumbuka!

Sio kila kitu unachokiona unafaa kukiiga. Baadhi ya mambo unafaa kuachia wataalamu.

Ngono za video/ponografia sio kwa hakika ukweli

Unapoangalia video za ngono, unaona vitu ambavyo watu wengi hawapitii katika maisha yao. Ngono zinazohusisha umati mkubwa wa watu, kufanya mapenzi na watu usiowajua au mapenzi ya kufichwa, kila kitu kinawezekana  kwa ngono za video.

Lakini kumbuka kuwa ngono za filamu si mapenzi ya kikawaida ni kama hadithi ya kukisiwa zakuzuwa hisia.

Lakini kumbuka kuwa usitarajie kuwa ngono tunayofanya ya kawaida itakuwa kama ile ambayo inafanyika katika mitando ya ngono au kanda za ngono.

Zaidi wote wanaofanya ngono katika kanda hizo wana miili mikubwa na mboro kubwa sana. Na wale waigizaji  huwa wembamba na matiti makubwa ikilinganishwa na wanawake wengine.

Na pia huwa na dawa za kufanya maziwa yao kuwa makubwa au hata kufanyiwa upasuaji wa wa urembo. Na je mpenzi wako hupiga kelele nyingi kama wale wa filamu za mapenzi au hata kumwaga kwa urahisi.

Kumbuka video za ngono hutengenezwa kwa ajili ya ndoto za wanaume na pia huonyesha jinsi wanaume wanavyojiskia. Na pia kwenye filamu hizi hakuna mtu anayevaa mpira wa kondomu.

Tahadhari kuwa magonjwa ya zinaa hayapumziki. Usiache wahusika wa ngono wakuongoze. Baadhi yao wamesema wamepata ukimwi kwa mara ya kwanza kupitia hizi ngono za filamu. Na wewe pia

Faida na hasara ya ngono

Je ni makosa kuangalia video za ngono

Shwari kabisa,  si wewe peke yako kama unafanya. Kawaida si makosa kujifurahisha nafsi na ngono za filamu au kutiwa tamaa ya kimapenzi na filamu au picha za mapenzi. Ni sawa tu almuradi unafahamu kuwa sio katika ulimwengu wa kawaida. Lakini kumbuka kuwa huezi kujua vile mwigizaji huyo wa kike anavyohisi.

Ujue kuwa ngono ya mitandaoni inaonyesha dhulma dhidi ya wanawake au hata wanawake wakidhalilishwa . Na kuwa wanawake wako tu hapo kuwafurahisha wanaume. Unaweza kufikiaria chochote unachotaka. Lakini kuna tofauti kubwa kati ya mambo ya kukisiwa na ukweli

Ngono za filamu zina athari mbaya. Unaweza kuanza kuharibu mahusaiano yako ya kimapenzi ya kiukweli kwa sababu unaanza kufurahia ngono zaidi ya mambo ya kiukweli. Na hapo unaanza kujaribu ili kuhakikisha inaonekana kama ngono ya mitandaoni. Ambayo kwa kweli haiwezi. Kama umeanza tabia ya kuangalia sana video za ngono na unahisi kutaka zaidi na zaidi ni wakati sasa wa kuacha tabia hiyo.

Je unaangalia ngono. Je umejaribu hayo unayoyaona. Je ilikuwaje

did you find this useful?

Tell us what you think

LoveMatters Africa

Blush-free facts and stories about love, sex, and relationships